Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika taarifa, wizara hiyo imesema mashambulizi hayo "yanajumuisha ukiukaji maradufu wa kanuni za sheria za kimataifa na zile za Mkataba wa Umoja wa Mataifa pamoja na maazimio muhimu kwa Lebanon na Syria."
Wizara hiyo imebainisha kuwa kimya cha jamii ya kimataifa na uungaji mkono wa Marekani umeupa kiburi utawala haramu wa Israel cha kuendelea na mashambulizi yake dhidi ya Syria.
"Serikali ya Syria inawaonya watawala wa taasisi ya Israel dhidi ya kuendelea ukiukaji wa wazi na wa kiholela wa Israel na mashambulizi ya jinai." Aidha Syria imeonya kuwa vitendo hivyo vya Israel vinaweza kuvuruga utulivu wa eneo na amani na usalama wa kimataifa.
Wizara hiyo pia imesisitiza kwamba mashambulizi ya "woga" yatakuwa na madhara makubwa kwa wahusika.
Taarifa hiyo pia imesisitiza haki ya Syria ya kutumia "njia zote halali" kujibu mashambulizi, na kuwawajibisha wale walio nyuma yake kuhusu "athari za hatari" za mashambulizi hayo.
342/